HATUA YA KUZUIWA NAIBU RAIS KUSAFIRI NCHINI UGANDA YAZIDI KUSHUTUMIWA.


Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia hatua ya kuzuiwa naibu rais William Ruto kusafiri nchini uganda kwa ziara ya kibinfasi.
Baadhi ya wakazi wa makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamekosoa hatua hiyo wakisema naibu rais William Ruto ni kiongozi wa hadhi ya juu serikalini na kumzuilia kusafiri nje ya nchi ni kumdhalilisha, huku wakidai kuwa huenda hatua hiyo ina malengo fiche.
Aidha wakazi hao wamesema kuwa huenda maswala kama haya yakapelekea migawanyiko miongoni mwa wananchi hali ambayo itahujumu amani inayoshuhudiwa nchini ikizingatiwa taifa linaekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.