HATUA YA KUONDOLEWA NEMBO ZA UDA CHEPARERIA YASHUTUMIWA VIKALI.


Viongozi wa chama cha UDA eneo bunge la Pokot kusini katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameshutumu hatua ya kuondolewa nembo ya wilbaro ya chama hicho iliyokuwa imewekwa eneo la Chepareria kwa maandalizi ya ziara ya naibu rais William Ruto katika kaunti hii.
Mmoja wa viongozi hao Ben Loyatum amesema kuwa licha ya tofauti za vyama, ni jambo la busara kwa kila mmoja kuheshima sera za chama kingine kwa ajili ya kudumisha umoja miongoni mwa wakazi na kuheshimu demokrasia ya vyama.
Aidha Loyatuma amewataka vijana katika kaunti hii kutokubali kutumika na wanasiasa kutatiza shughuli za wapinzani wao kwani huenda wakakabiliwa kisheria.
Wakati uo huo Loyatum amewataka wakazi wa eneo hilo kuendelea kuunga mkono chama cha UDA ili kumwezesha mgombea wao wa urais naibu rais William Ruto kushinda kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti.