HATUA YA KUHARAMISHA MCHAKATO WA BBI YAZIDI KUKOSOLEWA.
Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Pokot magharibi wamekosoa hatua ya majaji wa mahakama kuu kuharamisha mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia mpango wa upatanishi BBI.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Kapchok Peter Lokor, viongozi hao wamesema kuwa BBI ina manufaa makubwa kwa wakenya hasa kuongezwa mgao wa kaunti ambao hutolewa na serikali kuu hali ambayo itaimarisha maendeleo mashinani.
Wakati uo huo Lokor ametetea hatua ya bunge la kaunti hii kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba akikana madai ya kupitisha nakala ghushi ya mswada huo na kusema kuwa walipitia yaliyokuwa katika nakala hiyo kabla ya kuipitisha.