HATIMAYE GAVANA WA POKOT MAGHARIBI PROFESA JOHN LONYANG’APUO AJITOKEZA BAADA YA KUCHUKUA LIKIZO FUPI


Baada ya kutoweka kwa kipindi cha mwezi moja huku maswali mengi yakiulizwa na wakaazi wa Pokot Magharibi waliotaka kujua alipo gavana wao hatimaye gavana John Lonyangapuo amejitokeza akiwa ameandamana na wandani wake ambao ni mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing, Mjumbe wa Sigor Peter Lochakapong, mbunge wa Kacheliba Mark Lomunokal na mwakilishi wa kina mama Lilian Tomitom.
Gavana Lonyangapuo alingia mjini makutano kwa mbwembwe na ucheshi wake ambao wanachi walikua wameukosa kwa muda.
Gavana Lonyangapuo alitumia fursa hiyo kuwaeleza wakaazi wa Pokot Magharibi kwamba alikua kwenye likizo ya mwezi mmoja huku akiwasuta baadhi ya viongozi kaunti hii waliokua wakieneza propaganda kwamba wanapaswa kuheshimiana