HATIMA YA SPIKA MUKENYANG KUBAINIKA LEO HUKU VIONGOZI WAKIENDELEA KUSHUTUMU HOJA YA KUBANDULIWA KWAKE.


Bunge la kaunti ya Pokot magharibi linapotarajiwa leo kujadili hoja ya kumbandua spika wa bunge hilo Catherine Mukenyang, baadhi ya viongozi kaunti hii wameendelea kukashifu hatua hiyo wanayodai imechochewa kisiasa.
Wa hivi punde kukosoa hatua hiyo ni mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema bunge hilo halikufaa kumbandua Spika Mukenyang ikizingatiwa ana muda mchache kabla ya kujiuzulu baada yake kutangaza kugombea kiti cha mwakilishi kina mama kaunti hii katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Moroto amedai kuwa wabunge katika bunge hilo wamehongwa ili kumwondoa Mukenyang afisini.
Wakati uo huo Moroto amesema ingekuwa bora iwapo wabunge katika bunge hilo ambao ni wanachama wa vyama vya KANU na Jubilee kutii maagizo ya vyama vyao ambavyo vilionya dhidi ya hatua hiyo, na kujitenga na shinikizo za kumwondoa spika mamlakani.