HALI YAZIDI KUWA TETE KATIKA HOSPITALI YA KAPENGURIA


Serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi imeendelea kushutumiwa kwa kuitelekeza hospitali ya Kapenguria.
Seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio amesema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa muhimu vinavyopasa kutumiwa na madaktari hali inayopelekea wagonjwa kulazimishwa kununua baadhi ya vifaa kabla ya kuhudumiwa.
Poghisio amedai licha ya serikali ya kaunti hii kupokea mgao wa fedha wa kutosha kuendeleza shughuli zake sekta ya afya imeendelea kudorora huku akiapa kutolegea katika kuhakikisha serikali ya kaunti inatoa huduma bora kwa mwananchi.