HALI YA TAHARUKI INGALI IMETANDA ENEO LA KAPEDO TURKANA MASHARIKI


Hali ya taharuki bado imetanda katika eneo la Kapedo Turkana Mashariki baada ya afisa mkuu wa oparesheni wa kitengo cha GSU nchini Emmadau Tebakol kuuliwa kwa kupigwa risasi na watu wanaoshukiwa kuwa wa kaunti jirani.
Afisa huyo wa polisi alikuwa amezuru Kapedo ili kujadiliana na maafisa wa usalama wa eneo hilo jinsi ya kumaliza uhasama na alipokuwa akirejea Nairobi gari la RDU ambalo alikuwa ameliabiri lilishambuliwa katika daraja la Kapedo kule Ameyen na kuuliwa papo hapo.
Wabunge James Lomenen wa Turkan Kusini ,Ali Lokiru wa Turkana Mashariki na John Lodepe wa Turkana ya Kati waliokuwa wamezuru Kapedo kufariji familia za watu walioshambuliwa hivi majuzi walishindwa kuondoka katika eneo la hilo kutokana hofu ya kuvamiwa.
Hata hivyo viongozi hao sasa wanaitaka serkali kuu kuhakikisha kwamba inaimarisha usalama katika eneo hilo.