HALI YA TAHARUKI IMETANDA KATIKA ENEO LA CHESOGON MPAKANI PA KAUNTI YA MARAKWET NA POKOT MAGHARIBINg’ombe zaidi ya 300 wameibwa huku wakazi wawili wakiripotiwa kuuliwa na wengine kujeruhiwa baada ya wavamizi wanaoaminika kutoka kaunti jirani kuvamia eneo la chesogon mpakani pa kaunti hii na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet hiyo jana.
Akithibitisha kisa hicho naibu kamishina eneo hilo Naphtali Korir amesema kuwa wavamizi hao waliwavamia wafugaji waliokuwa wakilisha mifugo eneo la Chesogon ambapo kulikuwa na makabiliano makali hali iliyopelekea mmoja wa wafugaji kuaga dunia huku mwingine akifariki alipokuwa akikimbizwa hospitalini.
Hata hivyo hali hiyo ilidhibitiwa na maafisa wa polisi huku waliojeruhiwa katika kisa hicho wakiendelea kupokea matibabu.
Korir amesema kuwa kwa sasa maafisa wanaendeleza doria ili kudhibiti hali huku akitaja mzozo kuhusu malisho kuwa chanzo cha uvamizi wa mara kwa mara ambao unashuhudiwa eneo hilo.