HAKUNA NAFASI KWA WAHUDUMU WA AFYA WANAOGOMA

BUSIA


Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojamong amesema kuwa hakuna nafasi kwa wahudumu wa afya wanaohusisha madaktari na wauguzi wanaoshiriki mgomo kwenye kaunit ya Busia.
Akizungumza kwenye mkutano wa wasomi kutoka eneo bunge la Budalangi Ojamong amesema kuwa mgomo huo sio halali kwa wahudumu wa afya kwenye kaunti hiyo akisema kuwa serikali ya kaunti yake tayari imeangazia maslahi yao kikamilifu.
Ojamong ametishia kwamba huenda wakatangaza wazi nafasi za wauguzi na madaktari ambao wanashiriki mgomo huo.
Haya yanajiri huku Gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati amewahimiza wahudumu wa afya walio katika mgomo kurejea kazini huku magavana wakiendelea kuangazia namna ya kushughulikia maslahi yao.