HAKI ZA BINADAMU ZAKIUKWA ENEO LA TIATY KAUNTI YA BARINGO


Viongozi kutoka kaunti hii ya Pokot Magharibi wamelalamikia ukiukaji wa haki za binadamu kutokana na oparesheni kali ya polisi inayoendelea katika juhudi za kuimarisha usalama eneo la Tiaty kaunti ya Baringo.
Wakiongozwa na mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing’ na wa Tiaty William Kamket, viongozi hao wamesema kuwa wakaazi wamekosa huduma na bidhaa muhimu huku wanafunzi wakikosa kuendelea na masomo.
Wawili hao wametoa wito kwa serikali kufungua bara bara kwa kuondoa vizuizi barabarani ili kuruhusu wakaazi kupata nafasi ya kupokea chakula.
Haya yanajiri huku waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’I akitarajiwa kufika mbele ya kamati ya usalama siku ya jumanne wiki ijayo ili kutoa mwangaza kuhusiana na oparesheni hiyo.