GHARAMA YA MAISHA NCHINI YAZIDISHA VILIO.


Hisia mbali mbali zimeendelea kuibuliwa nchini kufuatia kuendelea kupanda gharama za bidhaa mbali mbali hasa za kimsingi.
Wakiongozwa na Richard poriot mkaazi wa mawingo road viungani mwa mji wa makutano, wakaazi katika kaunt hii ya pokot magharibi wameshutuma serikali kwa kuendelea kupandisha bei ya bidhaa muhimu nchini.
Wakaazi hao sasa wameisihi serikali kushusha bei ya vyakula kama vile mahindi kutoka shilingi 220 hadi shilling 80 kwani maisha yamekuwa magumu kupindukia.
Aidha madereva wa magari mjini makutano wakiongozwa na Samuel Yego wanalalama kuwa kutokana na gharama ya maisha, kazi yao imeathirika na hivyo kufanya maisha kuwa magumu zaidi akitoa wito kwa serikali kuteremsha bei ya bidhaa ili maisha yarejelee hali ya awali.