GAVANA WA TRANS NZOIA PATRICK KHAEMBA ATAKIWA KUKAMILISHI MIRADI YA MAENDELEO.


Mwakilishi wadi mteule katika bunge la kaunti ya Trans nzoia bi Magret Sabina Wanjala amemtaka gavana wa kaunti hiyo Patrick Simiyu Khaemba kumaliza miradi yote ya maendeleo aliyoianzisha jinsi alivyoagiza kwenye manifesto yake wakati alipokuwa akiwania ugavana wa kaunti hiyo kwa awamu ya pili.
Bi. Wanjala amedai baadhi ya miradi ikiwemo hospitali ya rufaa ambayo inajengwa yastahili kumalizwa na gavana Khaemba wakati anapojipanga kutamatisha hatamu yake ya uongozi.
Kiongozi huyo vilevile ameunga mkono mapendekezo ya kuwalipa marupurupu magavana naibu gavana na wawakilishi wa wadi akidai yasipuuziliwe mbali.

[wp_radio_player]