GAVANA WA POKOT MAGHARIBI AWAHAKIKISHIA WAKAAZI AHADI ZOTE ALIZOTOA WAKATI WA KAMPEINI


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi amewahakikishia wakazi wa kaunti hii kuwa atahakikisha anatekeleza ahadi ambazo alitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti mwaka huu.
Akizungumza wakati akikagua hali katika hospitali ya kapenguria, Kachapin amesema kuwa serikali yake itaipa kipau mbele sekta ya afya hasa katika kuhakikisha kwamba dawa za kutosha zinapatikana katika hospitali zote na zahanati za kaunti hii ya pokot magharibi.
Kachapin amesema kuwa itahakikisha serikali yake inatumia vyema raslimali ambazo kaunti hii inatengewa na serikali kuu kuboresha huduma hizo za afya ili kupunguza visa vya wagonjwa kutoka kaunti hii kutafuta huduma hizo katika kaunti zingine.
Wakati uo huo Kachapin amewaahidi wakazi wa kaunti hii utofauti mkubwa katika uongozi wake akisema sasa ana tajriba ya kutosha kuendesha maswala ya kaunti hasa baada ya kuhudumu kama gavana wa kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.