GAVANA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAHUDUMU WA AFYA HII LEO


Mkutano ulioratibiwa kufanyika hiyo jana wa Wahudumu Wa Afya kwenye kaunty hii ya Pokot Magharibi na haukufanyika unatarajiwa kurejelewa tena hii leo.
Hiyo jana gavana wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Pro John Lonyang’apuo aliahirisha mkutano huo kwa mara ya tatu sasa jambo linasubiriwa kwa hamu na gahamu iwapo atakutana na wahudumu hao au la.
Ikumbukwe kwenye kaunty ya Pokot Magharibi wahudumu wa kiliniki walisitisha mgomo wao tangu siku ya jumatatu wiki hii huku wakisubiri kukutana na maafisa wa afya wa kaunty hii ili kufanya majadiliano.
Haya yanajiri huku mgomo wa wauguzi na maafisa wa kliniki nayo ikiingia siku ya tatu leo hii huku athari zake katika sekta ya afya zikiendelea kudhihirika.
Hali hiyo imelazimika baadhi ya wagonjwa kuhama hospitali za umma na kusaka huduma katika hospitali za binafsi huku waliosalia hospitalini wakikosa huduma muhimu.

[wp_radio_player]