GAVANA WA KAKAMEGA AMTAJA MRIDHI WAKE MWAKA WA 2022


Huku siasa za uridhi wa kiti cha ugavana wa Kakamega zikionekana kungo’a nanga gavana wa kaunti hiyo dkt. Wycliffe oparanya amemtaka naibu wake prof. Philip kutima kutima kuanza kutafuta umaarufu wa kumridhi.
Oparanya amemtaka naibu wake kunoa makali kabla ya uchaguzi mkuu ujao, ili aweze kuchukua usukani baada ya muda wake wa kuhudumu kukamilika na kamwe hatavunja ahadi yake.
Huku akiwasuta wale wanaoeneza siasa za porojo kuwa huenda akamtema kutima , akisema atakuwa mstari wa mbele kumpigia debe kwenye uchaguzi mkuu ujao.