GAVANA LONYANGAPUO NA MBUNGE MOROTO WAHIMIZWA KUELEWANA KUHUSU MIRADI WATAKAYOTEKELEZA ILI KUZUIA KUKINZANA ENEO BUNGE LA KAPENGURIA.


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto wametakiwa kuketi chini na kuelewana kuhusu barabara watakazojenga katika eneo bunge hili ili kuzuia hali ya kukinzana kimajukumu.
Ni wito wake mwakilishi wadi ya Kapenguria Emmanuel Madi baada ya kila mmoja wa wawili hao kuahidi kujenga barabara ya chewoyet-tambo ambayo imepelekea kuathirika shughuli za uchukuzi kutokana na hali yake mbovu.
Wakati uo huo Madi ameapa kuwashinikiza viongozi hao kuhakikisha barabara mbovu katika wadi ya kapenguria zinakarabatiwa hasa baada ya kutengewa fedha za kutosha kufanikisha shughuli hiyo ili kuwaepusha wakazi na mahangaiko wanayopitia hasa msimu wa mvua.

[wp_radio_player]