GAVANA LONYANGAPUO AWAPUUZILIA MBALI WAPINZANI WAKE WA KISIASA


Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuyo amepuuzilia mbali madai yanayoendelezwa na wapinzani wake wa kisiasa kuhusu utendakazi wake katika kipindi ambacho amekuwa madarakani.
Gavana Lonyangapuo amesema kuwa hatojibizana na wanasiasa hao ila ataendelea kujihusisha na shughuli ya kuhakikisha anatimiza manifesto yake jinsi alivyowaahidi wakazi wa kaunti hii.
Aidha Lonyangapuo amesema ametekeleza mengi tangu alipochukua hatamu ya uongozi kama gavana wa kaunti hii, ikiwemo ujenzi wa barabara maeneo mbali mbali na sasa analenga kuhakikisha wakazi wanapata maji safi.