GAVANA LONYANGAPUO ATAKIWA KUWEKA WAZI MIRADI YA MAENDELEO ALIYOTEKELEZA.

Na Benson Aswani
Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo anapotarajiwa kugombea kiti hicho kwa muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, shinikizo zimeendelea kutolewa kwake kuweka wazi miradi ya maendeleo ambayo ametekeleza katika kipindi chake cha uongozi muhula wa kwanza.
Msemaji wa jamii ya sengwer kaunti hii ya Pokot magharibi Dickson Rotich amesema kuwa alipokuwa akitafuta uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, gavana Lonyangapuo alisema kuwa atazidisha mara tatu maendeleo aliyotekeleza gavana wa kwanza Simon Kachapin na sasa ni wakati anasatahili kuthibitisha kauli hiyo.
Wakati uo huo Rotich amemsuta gavana Lonyangapuo kwa kufeli kumchagua naibu gavana muda mrefu tangu kutengana na Nicholas Atudonyang akidai kuwa fursa hiyo ilifaa kupewa mtu kutoka jamii ya Sengwer kutokana na hali kuwa gavana mwenyewe ni kutoka jamii ya Pokot.