GAVANA LONYANGAPUO AKARI KUJITOLEA SERIKALI YAKE KUIMARISHA ELIMU POKOT MAGHARIBI.
Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amekariri kauli yake kuwa serikali yake imejitolea kuhakikisha kuwa kila mkazi wa kaunti hii anapata elimu.
Akizungumza wakati akizindua kontena za kufanyia biashara mjini Makutano, Lonyangapuo aidha ametoa hakikisho la kutimiza ahadi yake ya kuongeza kiwango cha fedha za basari hadi shilingi alfu 20 kwa kila mwanafunzi na kuwa hivi karibuni atatoa awamu ya pili ya fedha hizo.
Aidha Lonyangapuo amesema kuwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na taasisi za elimu imeongezeka pakubwa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kufuatia hatua yake ya kutoa fedha za basari kuwawezesha kuhudhuria masomo.
Wakati uo huo Lonyangapuo ametetea rekodi yake ya maendeleo tangu alipochaguliwa gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi.