GAVANA LONYANGAPUO AHUTUBIA WAKAAZI WA POKOT MAGHARIBI KUHUSIANA NA UTENDAKAZI WAKE


Gavana wa kaunti hii Prof. John Lonyangapuo amehutubia wakazi wa kaunti hii kuhusiana na utendakazi wake baada ya miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza baada ya hotuba yake bungeni katika kaunti hii ya Pokot Magharibi, Lonyangapuo amesema chumba cha wagonjwa mahututi kimejengwa na ki tayari kuzinduliwa wakati wowote kuanzia wiki ijayo.
Wakati uo huo ameendelea kuisifia miradi yake ikiwamo ujenzi wa chumba cha kuwashughulikia watu wanaougua ugonjwa wa figo pamoja na ugavi wa basari kwa wanafunzi wote wa sekondari katika kaunti hii huku akitoa ahadi ya kuongeza ugavi huo kuanzia mwaka ujao.