GAVANA KHAEMBA ATAKIWA KUFIKA MBELE YA KAMATI YA UHASIBU YA BUNGE LA TRANS NZOIA.


Kamati ya uhasibu katika bunge la kaunti ya Trans-nzoia ikiongozwa na mwenyekiti wake Peter Waswa ambaye pia ni mwakilishi wadi ya bidii wamemualika gavana Patrick Khaemba pamoja na maafisa wake wakuu kwenye kikao na kamati hiyo kufafanua kuhusu maswali ya muhasibu mkuu kuhusu matumizi ya fedha katika kaunti hiyo.
Kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge la kaunti hiyo, Waswa amesema miongoni mwa maswala yaliyoibuliwa na mhasibu mkuu wa serikali ni matumizi ya fedha katika ujenzi wa hospitali ya rufaa , unjezi wa soko jipya mjini kitale pamoja na utata katika sajili rasmi ya mali ya serikali ya kaunti yenye thamani ya shilingi b 8.

Aidha Waswa ameelezea kwamba iwapo gavana pamoja na maafisa wake wakuu watasusia mkutano huo basi italazimu kamati hiyo kufuata sheria na kumlazimu kufika mbele ya kamati hiyo kupitia mahakama na maafisa wa usalama kumwasilisha kwenye kikao hicho.