FORD KENYA YAFANYA KURA ZA MCHUJO ENEO BUNGE LA KABUCHAI


Chama cha Ford Kenya kimeandaa uchaguzi wake wa mchujo wa kutafuta atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa kuwania ubunge wa eneobunge la Kabuchai.
Katika kura hiyo ya mchujo Joseph Simiyu Majimbo ameibuka mshindi na ndiye atakeyekuwa mgombea wa Ford Kenya. Majimbo ameshinda baada ya kinyang’anyiro kikali akishindana na Eric Wanyonyi amabye alipata kura 32 zikilinganishwa na 70 alizopata Majimbo .
Mwaniaji mwengine Peter Kapanga alijiondoa ili kuwania akiwa mgombea huru.
Uchauguzi mdogo wa eneobunge la Kabuchai itafanyika mwezi Machi tarehe 4 kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo James Lusweti.