FORD KENYA CHAPATA PIGO HUKU DAP-K KIKIVUNA PAKUBWA TRANS NZOIA.


Chama cha Ford Kenya kimepata pigo baada ya waakilishi wadi kadhaa akiwemo David Kisaka wa Kiminini na Benard Mlipuko wa Kapomboi katika kaunti ya Trans nzoia kuhama chama hicho na kujiunga na DAP-K.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha waakilishi wadi hao, kiongozi wa chama cha DAP-K Wafula Wamunyinyi amesema kuwa viongozi hao wamevutiwa na mwamko mpya wa chama hicho katika kukuza demokrasia.
Wakati uo huo waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa aliyekuwepo katika hafla ya kuwapokea wawakilishi wadi hao amewahimiza wabunge kupitisha mswada wa marekebisho ya sheria za vyama mwaka 2021 ili kurahisisha mchakato wa kubuni miungano ya siasa.