FORD KENYA CHAPANGA KUWAFURUSHA WANACHAMA WAASI TRANS NZOIA.


Chama cha Ford Kenya katika kaunti ya Trans nzoia kimetangaza kuwatimua wanachama waasi waliochaguliwa kupitia chama hicho na nafasi zao kujazwa na viongozi waaminifu wakati kikijiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Mwanasheria wa chama hicho Benson Milimo ambaye pia ametangaza nia ya kugombea kiti cha ubunge eneo bunge la Cherang’ani amesema kuwa mikakati yote imewekwa ya kuwafurusha katika nyadhifa zao wanachama waasi ambao wametangaza kuunga mkono sera za vyama vingine.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Trans nzoia, mbunge wa Kwanza Ferdinand Wanyonyi anayesema kuwa wanachama hoa ndio wanaochochea migogoro ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika chama hicho.