‘FARASI NI WAWILI AGOSTI 9,’ ASEMA MULIPUKO.


Kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti kitakuwa baina ya farasi wawili hivyo vigogo wa muungano wa one Kenya alliance OKA wanafaa kutafakari kuhusu misimamo yao.
Haya ni kulingana na mwakilishi wadi ya Kapomboi katika kaunti ya Trans nzoia Benard Mulipuko ambaye amesema kuwa rais wa tano wa taifa hili atakuwa kati ya naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga hivyo ni sharti wakazi wa magharibi ya nchi wafanye uamuzi wa busara.
Kuhusu mswada wa marekebisho ya sheria za vyama vya kisiasa wa mwaka 2021 uliopitishwa bungeni, Mulipuko amesema kuwa japo mswada huo una manufaa mengi, changamoto ambazo zinamkumba mkenya wa kawaida ni sharti zifanywe kipau mbele.