FAMILIA BUSIA YALILIA HAKI BAADA YA MAHAKAMA KUWANYIMA HAKI


Familia moja kule Nambale kaunti ya Busia inalilia haki baada ya kesi dhidi ya maafisa wa polisi ambao wanadaiwa kuwadhulumu zaidi ya miezi 10 iliyopita kutupiliwa mbali.
Familia hiyo ya mzee Benard Orengo imesema kuwa ilivamiwa nyumbani kwao na kupiga hadi kuwajeruhi mnamo tarehe 30 mwezi machi mwaka jana na maafisa wa polisi kwa madai kwamba walikuwa wamekaidi amri ya kutokuwa kuwa nje.
Kisa hicho kilipelekea mamlaka ya kudhibiti utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA ilifanya uchunguzi dhidi ya maafisa 15 na maafisa wengine 6 lakini mashtaka dhidi yao yameondolewa.
Hussein Khalid ambaye ni mkurugenzi wa shirika la haki Africa amekashifu vikali hatua hiyo ya kuwaondolea mashtaka maafisa wa polisi huku akisema kuwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yataingilia kati ili kuhakikisha familia hiyo inapata haki.