EACC NA DCI YASHAURIWA KUKAGUA STAKABADHI ZA WAFANYIKAZI WA BUNGE LA KAUNTI YA TRANS NZOIA


Siku moja tu baada ya kamati ya haki na sheria katika bunge la kaunti ya Trans Nzoia kugundua dosari katika stakabadhi za waziri wa afya Clare Wanyama na kukosa kumuidhinisha kuwa mwanasheria mkuu wa kaunti hiyo, chama cha wafanyakazi wa kaunti hiyo sasa kimeirai tume ya maadili nchini EACC na idara ya upelelezi DCI kufanya ukaguzi wa wafanyakazi wote.
Wakiongozwa na mwenyekiti wake Kiboi amesema kwamba ukaguzi huo utawafichua wafanyakazi hewa na walioajiriwa kinyume na sheria za uajiri ili warejeshe fedha ambazo wamekuwa wakipokea kinyume na sheria.
Kadhalika amedokeza kwamba chama hicho na mashirika ya umma yataishtaka bodi ya kuwaajiri wafanyakazi wa umma kwa kukiuka sheria za utendakazi wake.
Hali hiyo imejiri baada ya Clare kukosa kuwasilisha vyeti vyake vya shule ya msingi wakati wa mchakto wa kuwahoji waliokuwa wakilenga wadhifa wa mwanasheria mkuu wa kaunti ya Trans Nzoia.