DKT SAMUEL POGHISIO ATETEA UTENDAKAZI WAKE KAMA SENETA WA POKOT MAGHARIBI


Seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi Dkt samuel poghisio ametetea utendakazi wake kama seneta wa kaunti hii tangia alipochaguliwa afisini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kanisa katoliki eneo la Nasukuta, Poghisio amesema kuwa tangu alipoingia afisini, fedha ambazo zinatumwa katika kaunti hii zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 4 hadi zaidi ya bilioni 7.
Hata hivyo Poghisio amesema licha ya juhudi zake kuhakikisha kaunti hii inapata mgao wa kutosha wa fedha, serikali ya kaunti haijaonyesha nia ya kuwajibikia fedha hizo, sekta mbali mbali hasa ya afya na ile ya elimu zikiwa zimetelekezwa.
Poghisio ameilaumu tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kwa ongezeko la ufujaji wa fedha za umma kaunti hii kwa kile amedai maafisa wake wameshindwa kuiwajibisha serikali ya kaunti hii.
Kadhalika amemtaka afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak kuwachunguza maafisa ambao hutumwa kuendesha uchunguzi huo.