DKT KARANJA KIBICHO ASHTUMIWA KWA MADAI YA KUTUMIA MAMLAKA NA AFISI YAKE VIBAYA


Mbunge wa Saboti Caleb Hamisi amamshutumu katibu wa kudumu katika wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho kwa kile ametaja kama kutumia mamlaka na afisi yake vibaya.
Akihutubu eneo bunge la Cherangani wakati wa kuipigia debe BBI, Hamisi amemtaka Kibicho kukoma kutumia maafisa tawala kushinikiza BBI kwa wananchi na badala yake kuwaachia viongozi na wanasiasa kuendeleza kampeni hiyo, akikosoa hatua hiyo kwakusema kuwa BBI ni swala la kisiasa wala sio maswala ya usalama wa ndani.
Nimatamushi yalioungwa mkono na kiongozi wa vijana Alex Matere akitaka safari nzima ya mabadiliko ya katiba kupitia mchakato wa BBI kuwahusisha vijana kikamilifu mbali na maswala muhimu ya vijana kutiliwa mkazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na fedha za kujikwamua kiuchumi.