DEMOKRASIA VYAMANI YATILIWA SHAKA.


Ni hatua chache mno zimepigwa ili kuafikiwa kwa demokrasia katika vyama vya kisiasa humu nchini.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la Haki na Amani Justice and Peace Kaunti ya Trans-Nzoia Leonard Barasa.
Akihutubu kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Demokrasia yaliyoandaliwa katika Kaunti ya Trans Nzoia, Barasa amesema vyama vingi vya kisiasa havitilii maanani maoni ya wanachama wa kawaida katika maamuzi muhimu kwenye vyama hivyo jambo ambalo limepelekea mambo muhimu ya vyama vya kisiasa kuwa majukumu ya watu wachache.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Immaculate Shamallah mkurugenzi wa muungano wa viongozi akina Mama Kaunti ya Trans Nzoia, akisema kumeshuhudiwa changa moto nyingi katika kuafikiwa kwa demokrasia kwenye uendeshwaji na usimamizi wa vyama vya kisiasa nchini, akisisitiza haja ya mabadiliko ili kuafikiwa demokrasia halisi nchini.