CHUO CHA KITALE CHA NATIONAL POLYTECHNIC KNP CHA TEUA RAIS MPYA MIONGONI MWA WANAFUNZI KAUNTI YA TRANSNZOIA

Dan Tanganyika ndiye Rais mpya wa chuo cha kitaifa cha Kitale national polytechnic (KNP) kufuatia uchaguzi ulioandaliwa katika chuo hicho.

Kwenye mkao na wanahabari baada ya kuapishwa rasmi Tanganyika ameahidi kushirikiana na usimamizi wa chuo hicho ili kuhakikisha Kuwa anabadili uongozi wa usimamizi wa wanafunzi chuoni humo.

Kwa Upande wake msimamizi mkuu wa chuo hicho John otieno Okola ameahidi kushirikiana na Uongozi mpya wa chuo hicho ili Kuhakikisha kuwa maslahi ya wanafunzi yanazingatiwa, akitoa wito kwa uongozi mpya wa chuo hicho kuhakikisha wanazingatia katiba ya wanafunzi wa chuo hicho.