CHUO CHA KITALAKAPEL CHALALAMIKIA UHABA WA MAJI.


Uongozi wa chuo cha kitalakapel katika kaunti hii ya Pokot magharibi umelalamikia ukosefu wa maji katika shule hiyo na eneo la Kitalakapel kwa ujumla.
Mwalimu mkuu chuo hicho john Kibowen amesema kuwa hali hiyo imefanya vigumu kuendeshwa shughuli katika chuo hicho na kuwa bwawa ambalo lilikuwa likichimbwa ili kutumika na chuo hicho lilikwama kufuatia kutokamilishwa malipo kwa mwanakandarasi aliyekuwa akitekeleza shughuli hiyo.
Amesema wanafunzi wa chuo hicho wanapoteza muda mwingi wakitafuta bidhaa hiyo muhimu ambapo wanazimika kutembea mwendo mrefu kuyatafuta.
Kibowen ametoa wito kwa viongozi kaunti hii akiwemo gavana John Lonyangapuo pamoja na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto kuingilia kati na kuhakikisha kuwa bidhaa hiyo muhimu inapatikana katika chuo hicho