CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI CHAKARIBIA KUKAMILIKA KATIKA HOSPITALI YA KAPENGURIA


Waziri wa afya kaunti hii ya Pokot magharibi Christine Apakoreng amesema kuwa chumba cha kuwahudumia wagonjwa mahututi katika hospitali ya kepunguria kimekaribia kukamilika.
Aidha Apakoreng amesema wahudumu wa afya ambao watakuwa wakihudumu katika chumba hicho tayari wamepewa mafunzo, na kwa sasa kinachosubiriwa ni baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika chumba hicho kabla ya kuanza kuhudumu.
Wakati uo huo apakoreng amesema kufikia sasa takriban wakazi alfu 3000 wa kaunti hii ya Pokot magharibi walio katika kundi la awamu ya kwanza ya utoaji chanjo dhidi ya virusi vya corona wamepokea chanjo hiyo ambayo inaendelea kutolewa kote nchini.