CHIFU WA NAMODO POKOT MAGHARIBI ASHUTUMIWA KWA UNYAKUZI WA ARDHI.


Wakazi wa kijiji cha Namodo eneo la Lokichar kaunti hii ya Pokot magharibi wameandamana kulalamikia kile wamedai hatua ya chifu wa eneo hilo kunyakua ardhi yao.
Wakazi hao wanamtuhumu chifu wa eneo hilo William Riamakira kwa kunyakua shamba lenye ekari 500 na kuwakodisha watu kuharibu na kuteketeza makazi yao.
Wakazi hao wamesema kuwa juhudi zao kutafuta haki zimekosa kuzaa matunda kutokana kile wamedai kuwa chifu huyo anatumia maafisa wa polisi kuwadhulumu.
Hata hivyo akijibu madai hayo chifu Riamakira amesema kuwa ardhi hiyo imekuwa ikimilikiwa na jamii tangu mwaka 2006, huku akiwalaumu wakazi hao kwa kunyakua kipande hicho cha ardhi.
Itakumbukwa kuwa mahakama ilitoa agizo la kusitishwa zoezi la kuhamishwa wakazi hao hadi pale kesi hiyo itakapoamuliwa.