CHIFU WA KASITEI ATETEA SHIRIKA LA NRT POKOT MAGHARIBI.


Naibu chifu wa eneo la Kasitei eneo la Turkwel katika kaunti hii ya Pokot magharibi Joseph Psiwa ametetea vikali shirika Northern Rangelands Trust NRT dhidi ya shutuma mbazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake na baadhi ya wakazi wa kaunti hii.
Akizungumza eneo la Turkwel, Psiwa amesema kinyume na inavyodaiwa, shirika hilo limewanufaisha wakazi wa kaunti hii pakubwa kwa miradi ya kilimo hali ambayo imewawezesha zaidi kiuchumi.
Aidha Psiwa amesema kuwa vijana wengi katika kaunti hii wameajiriwa na shirika hilo na kupelekea wengi wao kuasi uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo hali ambayo imepelekea utulivu maeneo mengi ya kaunti hii ya Pokot magharibi.