CHEMNO AKASHIFIWA KUDAI KUMILIKI ARDHI TRANS NZOIA.

Na Benson Aswani
Viongozi katika kaunti ya Trans nzoia wamekashifu vikali matamshi ya naibu gavana wa kaunti ya Uasin gishu Daniel Chemno dhidi ya wakazi wanaoishi katika ardhi moja eneo la Keiyo eneo bunge la Kwanza kaunti ya Trans nzoia aliyodai kuwa ni ya jamii yake.
Mwakilishi wadi ya Keiyo Emmanuel Waswa amekemea matamshi hayo akimtaka Chemno kukoma kutoa matamshi kama hayo aliyoyataja kuwa uchochezi kwani huenda yakaibua machafuko eneo hilo ambako kumeshuhudiwa amani kwa kipindi kirefu.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini, naibu gavana wa Uasin Gishu Daniel Chemno alidai kuwa ardhi hiyo ni ya jamii yake na kuwa ana cheti halali cha ardhi hiyo na kuzitaka jamii ambazo zinaishi katika ardhi husika kuondoka.