CHANJO DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA KUANZA KUTOLEWA HAPO KESHO KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Waziri wa afya kwenye kaunti hii ya Pokot Magharibi Jack Yaralima amesema kuwa dozi elfu 6 ya chanjo dhidi ya covid 19 tayari imewasili kwenye kaunti hii ya Pokot Magharibi na inatarajiwa kuanza kutolewa rasmi hapo kesho.
Akizungumza na kito hiki kwa njia ya simu, Dkt Yaralima amesema kuwa wahudumu wa afya watapewa kipaumbele kupokea chanjo hiyo akisema kuwa yeye atakuwa wa kwanza kuipokea.
Hata hivyo amesema kuwa wahudumu wa afya ambao watatoa chanjo hiyo kwa saa wanaendelea kupokea mafunzo kwenye mkahawa mmoja hapa mjini Makutano.