CHAMA KIPYA CHA KUP CHA KATALIWA POKOT MAGHARIBI NA VIONGOZI WA KAUNTI HIYO


Seneta wa Kaunti hii Daktari Samuel Poghisio ametoa msimamo wake waziwazi kuhusiana Chama Cha KUP ambacho kimezinduliwa hiyo jana katika Jiji la Nairobi akisema kwamba kamwe hatajihusisha na vyama vya kikabila sasa na hicho.
Poghisio amesisitiza kwamba Chama Cha KANU kingali thabiti na ni Chama kitakachowahusisha wakazi wa kaunti hii katika meza ya kitaifa akiwataka wakazi wote kupuuzilia mbali Chama Cha KUP iwapo wanatazamia kupata manufaa ya serikali kuu.
Amewataka vijana kujitenga na Chama hicho ambacho kimeasisiwa na watu wachache katika Kaunti hii na ambacho kinatazamia kuwanufaisha wawakilishiwadi pekee pamoja na gavana Lonyangapuo huku akiwataka vijana kujihusisha na vyama vya kitaifa ambavyo huenda vikawanufaisha zaidi kupitia ajira vikilinganishwa na chama cha nyumbani cha kikabila.
Wakati huo huo amemsuta gavana Lonyangapuo kwa kujihusisha na masuala yasiyowasaidia wakazi wa kaunti hii na kuyafumbia macho masaibu ya watu walioathirika na janga la maporomoko ya ardhi yaliyowakumba wakazi wa maeneo mbalimbali katika Kaunti hii.
Kuhusiana na hilo, Poghisio amesema Lonyangapuo amedinda kuwapa waathiriwa misaada waliyopewa na wahisani na badala yake amezihifadhi katika ofisi za kaunti watu wakiendelea kuumia.