CHAMA CHA UDA POKOT MAGHARIBI CHAIBUA MADAI YA KUTUMIKA FEDHA KUVURUGA MIPANGO YAKE.


Viongozi wa kisiasa ambao ni wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kukashifu kile wamedai kuwa baadhi ya viongozi katika kaunti hii wanatumia vijana kuvuruga mipango ya vyama vingine.
Wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Sook Martine Komongiro, viongozi hao wamemsuta gavana wa kaunti hii John Lonyangapuyo kwa madai ya kutumia raslimali za umma kuwalipa vijana kuendeleza vurugu hizo.
Wakati uo huo Komongiro amekosoa mipango ya maendeleo ya gavana Lonyangapuo kwa kile amedai kutoa kipau mbele kwa miradi isiyo muhimu kwa wakazi, miradi anayotumia kuendeleza ufisadi huku maswala muhimu yakisalia bila kushughulikiwa.
Komongiro ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti na kuwachuja viongozi wote waliotangaza nia za kugombea viti vya kisiasa ili kuwachagua wenye rekodi ya maendeleo na kuwafurusha wale wasiowajibika.