CHAMA CHA UDA CHAENDELEA KUPIGIWA UPATO POKOT MAGHARIBI


Viongozi mbali mbali wandani wa naibu Rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wameendelea kupigia upato chama cha UDA kinachohusishwa na Ruto wakikitaja kuwa suluhu kwa changamoto zinazowakumba wakenya.
Wakizungumza eneo la Kiwawa Pokot Kaskazini, viongozi hao wakiongozwa na mwakilishi kina mama kaunti hii Lilian Tomitom wamesema kuwa sera za chama hicho zinajali maslahi ya mwananchi wa kawaida huku wakimpigia upatu Ruto kutwaa uongozi wa taifa katika uchaguzi mkuu ujao.
Wakati uo huo Tomitom amesema kuwa kaunti hii ya Pokot Magharibi itanufaika pakubwa chini ya utawala wa chama cha UDA ikizingatiwa ni moja ya kaunti ambazo zimesalia nyuma kimaendeleo akitoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuunga mkono chama hicho.