CHAMA CHA KUP CHA CHA POKOT MAGHARIBI CHA CHAPISHWA KWENYE GAZETI RASIMI
Chama Kipya Cha Kenya Union Party KUP ambacho kimeasisiwa na gavana wa Kaunti ya Pokot Magharibi Profesa John Lonyangapuo kimechapishwa rasmi katika Gazeti la Kitaifa.
Akizungumza na kituo hiki, Naibu Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing’, amesema imefika wakati ambapo jamii ya Pokot kuwa na sauti yake katika meza ya kitaifa.
Kulingana na David Pkosing’ Gavana Lonyang’apuo ndiye atakuwa kinara wa Chama hicho huku yeye akiwa naibu Mwenyekiti.
Amesema viongozi katika chama hicho wanatarajiwa kutoka katika sehemu mbalimbali ya taifa hili huku akiwarai viongozi wa kaunti ya Pokot Magharibi kujitokeza kwa wingi kujiunga na Chama hicho.
Ameongeza kuwa uzinduzi wa Chama hicho Cha KUP unatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya maafikiano baina ya waanzilishi.
Kwa mjibu wa takwimu za msajili wa vyama anne nderitu sasa kuna vyama themanini na saba viivyosajiliwa rasimi