CHAMA CHA KITAIFA CHA WAZAZI KAUNTI YA TRANS NZOIA CHA PONGEZA AGIZO LA WIZARA YA ELIMU KWA WATAHINIWA WA DARASA LA NANE KUTEUWA UPYA SHULE ZA UPILI


Agizo la wizara ya elimu kwa watahiniwa wa darasa la nane kuteuwa upya shule za upili watakazo jiunga nazo kwenye kaunti ndogo, limepokelewa vyema na chama cha kitaifa cha wazazi kwenye kauti ya Trans Nzoia.
Mwenyekiti wa chama hicho Wellington Waliahula amesema kuwa hatua hiyo itatoa fursa mwafaka kwa wazazi kufuatilia miendendo ya wanao na kuwapa ushauri nasaha ili kukabili visa vya mioto shuleni.
Akizungumza na wanahabari mjini Kitale, Waliahula amesem akuwa wazazi wamekuwa wakigharamika mno kwa kuchanga fedha za kujenga upya majengo yaliyoteketezwa shuleni.
Hata hivyo wameitaka serikali kwa ushirikiano na wasimamizi wa shule kufanya uchunguzi wa kina ili kubainisha chanzo cha mikasa hiyo.
Wakati uo huo Waliahula ameitaka wizara ya elimu kuingilia kati na kuwachukulia hatua kali za kisheria wakuu wa shule ambao wanawatuma watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne nyumbani wanapokaribia kuifanya mitihani yao ya kitaifa.