CHAMA CHA KANU POKOT MAGHARIBI CHAPUUZILIA MBALI UWEPO WA MIGAWANYIKO MIONGONI MWA WAGOMBEA.
Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amepuuzilia mbali madai ya kuwepo migawanyiko miongoni mwa baadhi ya wagombea viti vya kisiasa kupitia chama cha KANU katika kaunti hii.
Akizungumza na kituo hiki poghisio amesema kuwa chama hicho kinaendesha shughuli zake kwa njia ya demokrasia na hasa wakati huu mchujo wa chama unaposubiriwa ili kuhakikisha chama hicho kinatwaa viti vingi vya uongozi baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Poghisio amewataka wafuasi wa KANU katika kaunti hii ya poko magharibi kuyapuuza madai hayo na kuendelea kuunga mkono chama.
Aidha Poghisio amesema kuwa chama hicho kitatumia mbinu mbali mbali za kuwatafuta watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwa viti mbali mbali katika uchaguzi mkuu ujao ikiwemo maelewano miongoni mwa wagombea, uchaguzi pamoja na kutumia umaarufu wa mgombea eneo analotaka kusimama.