CHAMA CHA KANU KITAPATA UUNGWAJI MKUBWA KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NDIO KAULI YAKE NAIBU GAVANA DKT ATUDONYANG
Viongozi wa chama cha KANU katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamesisitiza kuwa chama hicho kingali imara katika kaunti hii.
Akizungumza katika kikao kilichoandaliwa kujadili mikakati ya kukiimarisha zaidi chama hicho, naibu gavana kaunti hii Nicholas Atudonyang ameelezea imani ya chama hicho kutwaa viti vingi kaunti hii katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Aidha Atudonyang amekisifia chama hicho kuwa kilichopelekea uhuru wa taifa kando na kuwa mwanzilishi wa demokrasia ya vyama vingi nchini.
Atudonyang alikuwa akizungumza katika hafla ya chama cha Kanu kilipokuwa kikizindua manifesto yake katika hafla iliyoongozwa na kiongozi wa chama cha Kanu Gedion Moi .
Chama hicho kitaendeleza sera zake za awali za kuegeza katika kilimo,uchumi na kupunguza madeni na kukabili ufisadi miongoni mwa mengine.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Nick Salat amesema manifesto hiyo ndio itakuwa mwongozo wa katika kuingia makubaliano na vyama vingine.
Hata hivyo Salat alionekana kushinikiza kiongozi wao kusonga mbele na mpango wa kuungana na vyama vingine ,bila kujali wenzake katika Oka.