‘CHAMA CHA KANU KINGALI IMARA POKOT MAGHARIBI’ ASEMA POGHISIO.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amesema kuwa chama cha KANU katika kaunti hii sasa kitaimarika zaidi baada ya kuondoka baadhi ya wanachama anaodai kuwa walikuwa wakivuruga chama hicho.
Akizungumza na kituo hiki seneta Poghisio amesema kuwa chama hicho kiko tayari kutoa ushindani mkali kwa vyama vingine na kuwa tayari kipo na wagombea wa nyadhifa zote zinazowaniwa kaunti hii katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Wakati uo huo Poghisio amesema kuwa KANU pamoja na vyama tanzu vya muungano wa OKA vinaendeleza mazungumzo ya kushirikiana na vuguvugu la azimio la umoja linaloongozwa na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ili kuunda serikali ijayo baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Poghisio ametetea hatua ya chama hicho pamoja na muungano wa OKA kwa jumla kuazimia kufanya kazi na muungano wa azimio la umoja akisema kuwa ni kupitia hatua hiyo tu ambapo kutashuhudiwa umoja na usawa wa jamii zote nchini.