‘CHAMA CHA KANU KINGALI IMARA POKOT MAGHARIBI.’ ASEMA ATUDONYANG.


Chama cha KANU kingali imara katika kaunti hii ya Pokot magharibi licha ya kuibuka vyama mbali mbali kueleka uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Akizungumza na kituo hiki kutoka mjini Texas Marekani, naibu gavana Nicholas Atudonyang amesema kuwa huu ukiwa msimu wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu, vyama vingi vitaendelea kuibuka wagombea nyadhifa mbali mbali wakilenga kuvitumia kuwania nyadhifa hizo ila KANU ndicho chama kitakachobuni serikali ijayo.
Atudonyang amesema kuwa KANU kitasimamisha wagombea katika nyadhifa zote zinazowaniwa kaunti hii katika uchaguzi mkuu ujao akisema kuwa kikosi kiko imara licha ya kuondoka chamani aliyekuwa kiongozi wa chama hicho kaunti hii gavana john Lonyangapuo aliyebuni chama tofauti cha KUP.
Wakati uo huo Atudonyang amewataka wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kudumisha amani na kuheshimu demokrasia ya kila chama kaunti hii licha ya utofauti wa misimamo ya kisiasa, na kumpa kila mgombea wa wadhifa wa siasa nafasi ya kuuza sera zake bila kuvurugwa.