CHAGUZI ZILIZOAHIRISHWA MENEO MBALI MBALI NCHINI HATIMAYE ZAANDALIWA LEO.
Baada ya subira ya muda sasa wakazi wa eneo bunge la pokot kusini na kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanaungana na wakazi wa maeneo mengine nchini ambako chaguzi mbali mbali ziliahirishwa kuwachagua viongozi wao.
Maafisa wa tume ya uchaguzi iebc waliwasilisha jana vifaa vya uchaguzi katika maeneo manane ambapo uchaguzi unaandaliwa leo.
Afisa mkuu wa uchaguzi katika eneo bunge la kacheliba Wilson kimtai kipchumba alisema kuwa uchaguzi wa leo una utofauti mkubwa kabisa ikilinganishwa na uchaguzi uliopita wa tarehe tisa.
“uchaguzi huu una utofauti ambapo ni wa kiti kimoja pekee kwa hivyo hatuna kazi nyingi ikilinganishwa na ule wa tarehe 9 mwezi agosti. Tunatarajia kukamilisha shughuli hii haraka iwezekanavyo.” Amesema.
Baadhi ya wakazi katika kaunti ya baringo wamewarai wenyeji katika maeneo kutakakoandaliwa chaguzi hizo kuhakikisha kwamba wanadumisha amani na utulivu.
Wakiongozwa na kiplimo chepkong’a kutoka baringo ya kati, wakazi hao wanasema amani ambayo ilishuhudiwa baada ya uchaguzi wa agosti tisa inafaa idumu hata katika chaguzi zinazoandaliwa leo katika maeneo ya Kacheliba Pokot kusini na kaunti ya kakamega na mombasa maeneo mengine ambako kunaandaliwa chaguzi hizo.
Kiplimo amesema kuwa itakua bora kwa kila mpiga kura kurejea nyumbani baada ya kushiriki katika zoezi hilo ili kusubiri matokeo yatakayotangazwa na maafisa wakuu wa kusimamia chaguzi hizo.
“Nawaomba wakenya katika maeneo ya Kacheliba, Pokot Kusini, Kakamega, Mombasa, Rongai na maeneo mengine kudumisha amani katika kipindi hiki ambapo kunaandaliwa uchaguzi. Wapige kura na kuelekea nyumbani ili wasubiri matokeo.” Amesema Kiplimo.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na nicholas cherogony ambaye ameutaja uchaguzi uliopita kuwa wa amani na kuwataka wakenya kuwa watulivu wanaposubiri mahakama ya juu kuskiza kesi za kupingwa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa tarehe 15 mwezi agosti na mwenyekiti wa iebc wafula chebukati.
Itakumbukwa kwamba mahakama ina hadi tarehe 5 septemba kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliowasilishwa na chama cha azimio- one kenya.