CALEB AMISI ATEULIWA MWENYEKITI WA ODM TRANS NZOIA


Chama cha ODM tawi la Trans Nzoia kimemteua Caleb Amisi ambaye pia ni mbunge wa saboti kuwa mwenyekiti mpya chama hicho.
Kwenye mkao na wanahabari baada ya uteuzi huo uliowahusisha wanachama wakuu 20 kutoka kila maeneo bunge tano wakingozwa na John Simiyu wameelezea matumaini makubwa ya uongozi mpya wa chama hicho kukiimarisha na kumpigia debe kinara wa ODM Raila Odinga kupata uungwaji mkono mkubwa Kaunti hiyo na kutwaa urais mwaka wa 2022.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Washington Ngesa wakitaka mwenyekiti mpya kuhakikisha umoja wa chama hicho mbali na kuanzisha mikakati ya kukipigia debe chama cha ODM kwa kuwarai vijana kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura na wanachama wa chama hicho.