BUNGOMA LIBERATION LATAKA GAVANA WA BUNGOMA KUCHUNGUZWA


Vuguvugu la Bungoma liberation linataka gavana wa kaunti ya Bungoma Wyclife Wangamati kufanyiwa uchunguzi kufuatia matamshi yake kuwa ana damu ya kikundi cha FERA na atawaandama waakilishi wadi wanaopinga mipango yake ya kuwaajiri wasimamizi wa vijiji.

Kiongozi wa vuguvugu hilo Zakaria Barasa amedai kuwa siku moja tu baada ya gavana Wangamati kutoa matamshi hayo wanachama wa kikundi hicho walimvamia mwakilishi wadi ya Bumula ambapo walimuumiza vibaya na kuliharibu gari lake.

Barasa sasa anadai huenda usalama wa waakilishi wadi wengine wanaopinga mpango huo wa gavana Wangamati uko hatarini huku akitaka watu waliomvamia mwakilishi wadi huyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Aidha amemtaka gavana Wangamati kujitokeza wazi na kuelezea uhusiano wake na kundi hilo la FERA ambalo amelitaja kuwa kundi haramu.