BUNGE LA TRANS NZOIA LAPITISHA MAKDIRIO YA BAJETI YA 2021/2022.


Bunge la kaunti ya Trans nzoia hatimaye limepitisha makadirio ya bajeti ya kima cha shilingi bilioni 8.4 ya mwaka wa kifedha 2021/2022 na kumaliza mvutano wa kutotumia fedha hizo ambao umedumu kwa takriban miezi miwili baina ya serikali ya kaunti na bunge.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha uchumi na mipangilio David Kisaka amesema ni sharti kila wizara ilipe malimbikizi ya madeni ambayo yanakadiriwa kuwa shilingi bilioni moja kabla ya kufanikisha miradi ya maendeleo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Kinyoro Lawrence Mokosu na mwanachama wa kamati ya fedha mwakilishi wadi ya motosiet Benard Aliang’ana.